´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn


Mwanzo wa kitabu

Utangulizi 

 
 
 
 


 
Matunda ya ´Aqiydah hii

Namna ya kukaa Tashahhud katika Rakaa´ ya tatu na ya nne

Namna ya kukaa Tashahhud katika Rakaa´ ya tatu na ya nne

14- Ikiwa swalah ni ya Rakaa´ tatu, kama Maghrib, au ya Rakaa´ nne kama Dhuhr, ´Aswr na ´Ishaa atasoma Tashahhud iliyotanguliwa kutajwa punde tu [baada ya Rakaa´ mbili] pamoja na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) halafu atasimama hali ya kujisaidiza kwa kushika mapaja yake na wakati huo huo ainyanyue mikono yake sawa na mabega yake na huku aseme

"Allaahu Akbar" na aiweke mikono yake juu ya kifua chake - kama tulivyotangulia hapo juu - na asome "al-Faatihah" peke yake. Baadhi ya nyakati katika swalah za Rakaa´ tatu na nne baada ya kusoma "al-Faatihah"

akisoma Suurah nyingine ni sawa. Kumethibiti yanayofahamisha hivo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia Hadiyth ya Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh). Endapo ataacha kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya Tashahhud ya kwanza ni sawa. Kwa sababu imependekezwa na sio jambo la wajibu katika Tashahhud ya kwanza.

Baada ya Rakaa´ ya tatu atakaa Tashahhud [ya mwisho] ikiwa ni Maghrib na [atakaa Tashahhud] baada ya Rakaa´ ya nne ikiwa ni Dhuhr, ´Aswr na ´Ishaa - kama ilivyotangulia katika swalah za Rakaa´ mbili - kisha amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aombe kinga kutokamana na adhabu ya Moto, kaburi, fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal na akithirishe kuomba du´aa, kama yalivyotangulia hayo katika swalah ya Rakaa´ mbili. Lakini katika kikao hichi anatakiwa kukaa kitako cha Tawarruk. Nacho ni kuuweka mguu wake wa kushoto chini ya mguu wake wa kulia na makalio yake ayakaze juu ya ardhi
na wakati huo huo mguu wake wa kulia awe ameusimamisha kutokamana na

Hadiyth ya Abu Humayd juu ya hilo. Kisha atoe Salaam upande wa kulia na wa kushoto hali ya kusema:

"as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah."

Halafu amuombe Allaah maghfirah mara tatu. Baada ya hapo atasema:

} ال نت ال لام منك ال لام تبا كت ا الجلال الإك ام {

"Allaahumma antas-Salaam, wa minkas-Salaam, tabaarakta yaadhal-Jalaal wal-Ikraam."

"Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umetukuka ewe Mwenye utukufu na Mwenye kustahilki kuheshimika." (Muslim (591), at-Tirmidhiy (300), Abu Daawuud (1512), Ibn Maajah (928), Ahmad (05/280) na ad-Daarimiy (1348).)

kabla ya kuwaelekea watu iwapo atakuwa ni imamu. Kisha aseme:

} لا لو لا ا ه للّ حده لا ش يك لو، لو الم ك لو الح د ى ع ى كل شي دي ، ال لا مانع لما عطيت لا معطي لما منعت لا ينفع ا
الجد منك الجد، لا ح ل لا ة لا بالله، لا لو لا ا ه للّ لا نعبد لا ه لو النع ة لو الفضل لو الثنا الح ن لا لو لا ا ه للّ مخ ل لو
الدين ل ك ه ال ا ن {

"Laa ilaaha illa Allaah, wahdahuu laa shariyka lah, lahul-Mulk wa lahul-Hamd wa huwaa ´alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa hawla wa laa quwwatah illa billaah. Allaahumma laa maaniy´ limaa a´twayt, wa laa mu´twiya limaa mana´t, wa laa yanfau´ dhal jaddi mink al-Jadd. Laa hawla wa laa quwwatah illa billaah, laa ilaaha illa Allaah, wa laa na´abudu illa iyyaah, lahun-Ni´mah wa lahul- Fadhwl, wa lahuth-Thanaa´ al-Hasan. Laa ilaaha illa Allaah, mukhliswiyna lahud-Diyn, wa lau karihal-Kaafiruun."

"Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ufalme ni wa Kwake na himdi ni Zake Naye juu ya kila jambo ni muweza. Hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Ee Allaah! Hapana awezae kukizuia ulichokitoa na kukitoa ulichokizuia - wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani Kwako wewe ndio utajiri. Hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah, hatumuabudu mwengine asiyekuwa Yeye, neema na fadhila na sifa nzuri zote ni Zake. Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kumtakasia Yeye dini ijapokuwa watachukia makafiri." (al-Bukhaariy (808), Muslim (593), an-Nasaa´iy (1341), Abu Daawuud (1505), Ahmad (04/250) na ad-Daarimiy (1349).)

Aseme "Subhaan Allaah" mara thelathini na tatu, "Alhamdu lillaah" mara thelathini na tatu, "Allaahu Akbar" mara thelathini na tatu kisha atimize mia kwa kusema

"Laa ilaaha illa Allaah illa Allaah, wahdahuu laa shariyka lah, a wa lahul- Hamd wa huwaa ´alaa kulli shay-in Qadiyr." Baada ya hapo asome Aayat-ul- Kursiy, Suurah "al-Ikhlaasw", "al-Falaq" na "an-Naas". Afanye hivi baada ya kila swalah. Imependekezwa kukariri Suurah hizi mara tatu-tatu baada ya swalah ya Fajr na Maghrib. Kumepokelewa Hadiyth juu ya hayo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Adhkaar zote hizi ni Sunnah na sio faradhi.

15- Imependekezwa kwa kila Muislamu mwanaume na mwanamke kuhifadhi Rakaa´ kumi na mbili anapokuwa katika hali isiyokuwa ya usafiri. Nazo ni kuswali kabla ya Dhuhr Rakaa´ nne na Rakaa´ mbili baada yake, Rakaa´ mbili baada ya Maghrib, Rakaa´ mbili baada ya ´Ishaa na Rakaa´ mbili kabla ya Fajr.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizihifadhi katika hali isiyokuwa ya usafiri. Kuhusu anapokuwa katika hali ya usafiri alikuwa haziswali isipokuwa Sunnah ya Fajr na Witr. Hakika hizi mbili Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizihifadhi katika anapokuwa safarini na
asipokuwa safarini. Lililo bora ni kuziswali Raatibah hizi na Witr nyumbani.

Lakini hata hivyo akiziswali msikitini pia ni sawa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Swalah bora ya mtu ni ile anayoswali nyumbani kwake isipokuwa zile za faradhi." (al-Bukhaariy (689), Muslim (1301) na at-Tirmidhiy (412).)

Kuhifadhi swalah hizi ni miongoni mwa sababu zinazompelekea mtu kuingia Peponi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Anayeswali Rakaa´ kumi na mbili mchana na usiku, basi Allaah atamjengea nyumba Peponi." (Muslim (1198-1199), Abu Daawuud (1059) na an-Nasaa´iy (1773).)

Endapo ataswali Rakaa´ nne kabla ya ´Aswr, Rakaa´ mbili kabla ya Maghrib na Rakaa´ mbili kabla ya ´Ishaa ni jambo zuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Atakayehifadhi Rakaa´ nne kabla ya Dhuhr na Rakaa´ nne baada yake, basi Allaah (Ta´ala) atamharamishia Moto.
"(at-Tirmidhiy (393), Abu Daawuud (1077) na Ahmad (25547).)

Ina maana ya kwamba akizidisha Rakaa´ mbili baada ya Dhuhr - kwa sababu Sunnah ya Raatibah ni nne kabla yake na mbili baada yake - basi atakuwa amefikia kile kilichotajwa katika Hadiyth ya Umm Habiybah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Allaah ndiye anayeongoza katika mafanikio.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad bin ´Abdillaah, kizazi chake na Maswahabah zake na wenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah

Namna ya kukaa katika Tashahhud ya pili

Namna ya kukaa katika Tashahhud ya pili

13- Ikiwa swalah ni ya ni Rakaa´ mbili, kwa mfano swalah ya Fajr, Ijumaa na ´Iyd, baada ya kuinuka kutoka katika Sajdah ya pili atakaa hali ya kusimamisha mguu wake wa kulia na wakati huo huo ameulaza mguu wake wa kushoto na huku ameuweka mkono wake wa kulia juu paja lake la kushoto na amekunja vidole vyake vyote isipokuwa kidole cha shahaadah. Kidole hicho anatakiwa kuashiria Tawhiyd. Akikunja kidole cha mwisho na kidole cha pete kisha akakutanisha kidole gumba na kidole kirefu halafu akaashiria kidole cha shahaadah ni bora zaidi. Sifa zote mbili zimethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lililo bora Zaidi afanye hili wakati fulani na hili wakati mwingine. Aweke mkono wake wa kushoto juu ya paja na goti lake la kushoto kisha asome Tashahhud katika kikao hichi:

} ال يات لله الل ات الطيبات، ال لام ع يك ي ا النبي حمة الله ب كاتو، ال لام ع ينا ع ى عباد الله اللالح ، ش د ن لا لو لا
ا ه للّ ش د ن مح دًا عبده و لو، ثم يق ل ال صل ع ى محمد ع ى ل محمد ك ا ص يت ع ى ب اىي ل ب اىي نك حميد مجيد، با ك
ع ى محمد ع ى ل محمد ك ا با كت ع ى ب اىي ل ب اىي نك حميد مجيد {

"at-Tahiyyaatu lillaahi was-Swalawaatu wat-Twayyibaat. as-Salaam ´alayka ayyuha an-Nabiyy wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh. as-Salaam ´alaynaa wa ´alaa ´ibaadi llaahi as-Swaalihiyn. Ashhaduu allaa ilaaha illa Allaah wa ash-haduu anna Muhammadan ´abduhuu wa Rasuuluh."

"Maamkuzi mema na swalah na mazuri yote ni kwa Allaah. Amani ziwe juu yako, ee Mtume, na rehema za Allaah na baraka Zake. Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wa Allaah walio wema. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja na ni Mtume Wake."

Kisha aseme:

)ال صل ع ى محمد ، ع ى ل محمد ، ك ا ص يت ع ى ب اىي ع ى ل ب اىي ، نك حميد مجيد ، با ك ع ى محمد ،
ع ى ل محمد ، ك ا با كت ع ى ب اىي ، ع ى ل ب اىي نك حميد مجيد(

"Allaahumma swalli ´alaa Muhammad, wa ´alaa aali Muhammad, kamaa swalayta ´alaa Ibraahiym, wa ´alaa aali Ibraahiym, innaka hamiydun majiyd, wa baarik ´alaa Muhammad, wa ´alaa aali Muhammad, kamaa barrakta ´alaa Ibraahiym, wa ´alaa aali Ibraahiym, innaka hamiydun majiyd."

"Ee Allaah! Mswalie Muhammad na familia ya Muhammad kama Ulivyomswalia Ibraahiym na familia ya Ibraahiym - hakika Wewe ni muhimidiwa mtukufu - na mbariki Muhammad na familia ya Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na familia ya Ibraahiym - hakika Wewe ni muhimidiwa mtukufu."(al-Bukhaariy (797), Muslim (402), at-Tirmidhiy (1105), an-Nasaa´iy (1298), Abu Daawuud (968), Ibn Maajah (899), Ahmad (01/428) na ad- Daarimiy (1340).)

Halafu aombe kinga dhidi ya mambo mane kwa kusema:

} ال ني ع بك من ع اب ن من ع اب القبر من نة المحيا الم ات من نة الم يح الد ال {

"Allaahumma inniy a´udhubika min ´adhabi jahannam, wa min ´adhab al-Qabr, wa min fitnat-il-Mahyaa wal-Mamaat, wa min fitnat-il-Masiyh ad-Dajjaal."

"Ee Allaah! Naomba unikinge kutokamana na adhabu ya Moto na kaburi na kutokamna na fitina za uhai na kifo na kutokamana na fitina za al-Masiyh ad- Dajjaal."(al-Bukhaariy (1311), Muslim (588), at-Tirmidhiy (3604), an-Nasaa´iy (5513), Abu Daawuud (983), Ibn Maajah (909), Ahmad (02/454) na ad- Daarimiy (1344).)

Kisha aombe anachokitaka katika kheri za duniani na Aakhirah. Akiwaombea wazazi wake wawili au waislamu wengine du´aa ni sawa. Ni mamoja iwe swalah ni ya faradhi au ya Sunnah. Halafu atoe Salaam upande wa kulia na wa kushoto hali ya kusema:

"as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah."

Namna ya kukaa baina ya Sijdah mbili

Namna ya kukaa baina ya Sijdah mbili

10- Anyanyue kichwa chake na huku akisema "Allaahu Akbar" na auinamishe mguu wake wa kushoto na auikalie na wakati huo huo asimamishe mguu wa kulia na aweke mikono yake juu ya mapaja na magoti yake na aseme:

"Rabb Ighfir liy, wahdiniy, warhamniy, warzuqniy, wa ´aafiniy na wajburniy."

"Ee Mola! Nisamehe, uniongoze, unihurumie, uniruzuku, nipe afya na uniunge." (at-Tirmidhiy (284), Abu Daawuud (850) na Ibn Maajah (898).)

Anatakiwa awe na utulivu katika kikao hichi.

11- Asujudu Sijda ya pili na huku akisema "Allaahu Akbar" kisha afanye yale yale aliyofanya katika Sajdah ya kwanza.

12- Ainue kichwa chake na huku akisema "Allaahu Akbar" na akae kikao khafifu kama mfano wa kikao baina ya Sajdah mbili. Hiki huitwa kuwa ni "kikao cha kustarehe" ambacho kimependekezwa kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanachuoni. Endapo atakiacha hakuna neno. Katika kikao hichi hakuna Dhikr wala du´aa. Kisha asimame/apande kwenda katika Rakaa´ ya pili hali ya kujisaidiza kwa kushika mapaja - ikiwa kuna urahisi wa kufanya hivo - lasivyo ajisaidize kwa ardhi. Halafu asome "al-Faatihah" na kilicho chepesi kwake katika Qur-aan baada ya al-Faatihah. Ataendelea kufanya kama alivyofanya katika Rakaa´ ya kwanza.

Sujuud, kuinuka kutoka katika Sujuud na yenye kuhusiana nayo

Sujuud, kuinuka kutoka katika Sujuud na yenye kuhusiana nayo

9- Asujudu na wakati huo huo aseme "Allaahu Akbar" na huku atangulize magoti kabla ya mikono yake - iwapo kutakuwa urahisi wa kufanya hivo - la sivyo atangulize mikono yake kabla ya magoti yake. Vidole vya miguu na mikono yake vinatakiwa kuelekea Qiblah na vilevile aachanishe vidole vya mikono yake. Anatakiwa kusujudu juu ya viungo vyake saba: paji la uso, pua, mikono yake miwili, magoti yake mawili na matumbo ya vidole vya miguu yake. Halafu aseme:

"Subhaana Rabbiy´ al-A´laa"

"Utakasifu ni wa Mola, Aliye juu."

Akariri hivo mara tatu au zaidi.

Imependekezwa kuongezea juu yake:

"Subhaanaka, Allaahumma Rabbanaa wa bihamdik. Allaahumma Ighfir liy."

"Ee Mola! Utakasifu na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe." (al-Bukhaariy (761), Muslim (484), an-Nasaa´iy (1122), Abu Daawuud (877), Ibn Maajah (889) na Ahmad (06/43).)

Vilevile aombe du´aa kwa wingi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

amesema:

"Katika Rukuu´ muadhimisheni Mola. Ama katika Sujuud jitahidini katika kuomba du´aa, kwani kuna matarajio mkaitikiwa."(Muslim (738), Abu Daawuud (742), Ahmad (1260) na (1801).)

Ajiombee kwa Mola Wake yeye du´aa na awaombee vilevile waislamu wengine mema ya duniani na ya Aakhirah. Afanye hivi sawa katika swalah ya faradhi na ya Sunnah. Anatakiwa vilevile kutanua mikono yake mbali na mbavu zake, tumbo mbali na mapaja yake, mapaja mbali na miguu yake na asiinamishe mikono yake juu ya ardhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Nyookeni katika Sujuud na wala mmoja wenu asiinamishe mikono yake kama inavyofanya mbwa."(al-Bukhaariy (779), Muslim (762) na an-Nasaa´iy (1098).)