Takbiyrat-ul-ihraam

Takbiyrat-ul-Ihraam, kunyanyua mikono wakati wa Takbiyrah na kufunga mikono

3- Alete Takbiyrat-ul-Ihraam kwa kusema "Allaahu Akbar" na huku ni mwenye kutazama pahali pa kusujudia.

4- Pale anaposema "Allaahu Akbar" ainyanyue mikono yake sawa na mabega yake au na masikio yake.

5- Aiweke mikono yake juu ya kifua chake, kitanga cha kulia akiweke juu ya kitanga cha kushoto. Hilo ni jambo limethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).