kuelekea qibla

Kuelekea Qiblah

2- Mswalaji atanatakiwa kuelekea Qiblah ambapo ni Ka´bah popote alipo.

Anatakiwa kuuelekeza Qiblah mwili wake wote na huku anuie kwa moyo wake kutekeleza swalah ile anayotaka kuswali - ni mamoja iwe ya faradhi au ya Sunnah - na asitamke nia kwa ulimi wake. Kwa sababu kutamka nia kwa ulimi wake haikuwekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo kutamka nia wala Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum).

Imesuniwa kuweka Sutrah ambapo ataswali kwa kuielekea. Hili linamuhusu imamu au anayeswali peke yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kufanya hivo.