duaa ya kufungulia sala

Du´aa ya kufungulia swalah

6- Imesuniwa kusoma du´aa ya kufungulia swalah. Nayo ni:

} ال باعد بيني ب خطا ي ك ا باعدت ب المش ق المغ ب، ال نقني من خطا ي ك ا ينقى الث ب الأبيض من الدنس، ال
اا ني من خطا ي بالما الث ج البرد

"Allaahumma baa´id bainiy wa baina khatwaayaayaa kamaa ba´atta bainal-Mashriq wal-Maghrib. Allaahumma naqqiniy min khatwaayaayaa kamaa yunaqqaa thawb al-Abyadhw minad-Danas. Allaahumma ighsilniy min khatwaayaayaa bil-Maa´ wath-Thalj wal-Barad... "

"Ee Allaah! Niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Ee Allaah! Nitakase kutokamana na madhambi yangu kama vile inavyotakaswa nguo nyeupe na uchafu. Ee Allaah! Nisafishe kutokamana na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu... "

Vilevile akipenda badala ya du´aa hiyo anaweza kusoma ifuatayo:

وب انك ال بح دك تبا ك اسمك تعا دك لا لو ايرك
 {

"Subhaanak Allaahumma wa bihamdik, wa tabaaraka-ismuk, wa ta´aalaa jadduk, wa laa ilaaha ghayruk."

"Utakasifu na himdi zote ni Zako, limetukuka jina Lako, utukufu ni Wako na hapana mungu wa haki asiyekuwa Wewe."


Akisoma du´aa zingine za kufungulia swalah mbali na hizo mbili ni sawa.

Lililo bora zaidi ni wakati fulani asome hii na wakati mwingine asome nyingine. Huku ni kufuata kikamilifu zaidi. Baada ya hapo aseme:

"A´udhu billaahi min ash-Shaytwaan ar-Rajiym. Bismillaahi ar-Rahmaan ar-Rahiym."

"Ninajilinga kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyetiwa mbali na Rahmah zaa Allaah, kwa jina la Allaah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu."

Kisha asome Suurah "al-Faatihah". Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Hana swalah yule ambaye hakusoma mama wa Kitabu."4


Atapomaliza kuisoma aseme:

"Aamiyn".

Aseme hivyo kwa sauti ya juu ikiwa ni katika swalah za kusoma kwa sauti.

Akimaliza kusoma "al-Faatihah" asome kile kitachomkuia chepesi katika Quraan.