´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn


´Aqiydah yetu

´Aqiydah yetu ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake, siku ya Mwisho na Qadar; kheri na shari yake.

Tunaamini Uola wa Allaah (Ta´ala). Bi maana ya kwamba Yeye ndiye Mola, Muumbaji na Mfalme mwenye kuendesha mambo yote.

Tunaamini Uungu wa Allaah (Ta´ala). Bi maana Yeye ndiye Mungu wa haki na kila kinachoabudiwa badala Yake ni batili.

Tunaamini Majina na Sifa Zake, ina maana ya kwamba Yeye ana Majina mazuri na Sifa kamilifu zilizo kuu.

Tunaamini kuwa Yeye ni Mwenye kupwekeka katika mambo hayo. Bi maana hana mshirika katika Uola Wake, Uungu Wake wala katika Majina na Sifa Zake.

Allah (Ta´ala) amesema:


رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَہُمَا فَٱعۡبُدۡهُ وَٱصۡطَبِرۡ لِعِبَـٰدَتِهِۦ‌ۚ هَلۡ تَعۡلَمُ لَهُ ۥ سَمِيًّ۬ا 

"Mola wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua [mwengine] mwenye Jina kama Lake?"(19:65)


ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُ‌ۚ لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬‌ۚ لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِ‌ۗ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦ‌ۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ‌ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡ عِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَ‌ۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ‌ۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَا‌ۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ


"Allaah, hakuna mungu wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu. Haumchukuwi usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai [anayeombea] mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ndiye Aliye juu, ndiye Mkuu." (02:255)

هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ‌ۖ عَـٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ‌ۖ هُوَ ٱلرَّحۡمَـٰنُ ٱلرَّحِيمُ (٢٢) هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡقُدُّوسُ ٱلسَّلَـٰمُ ٱلۡمُؤۡمِنُ ٱلۡمُهَيۡمِنُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡجَبَّارُ ٱلۡمُتَڪَبِّرُ‌ۚ سُبۡحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشۡرِڪُونَ (٢٣)


”Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna mungu wa haki ila Yeye. Mjuzi wa yaliyofichikana na ya dhahiri, Yeye Ndiye Mwingi wa Rahmah, Mwenye kurehemu, Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye amani, Mwenye kusadikisha, Mwenye kutawala na kuendesha, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye kustahiki kiburi - Utakasifu ni wa Allaah kwa yale yote wanayomshirikisha nayo. Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Mtengeneza sura, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamtukuza Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi - Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima, Mwenye hikmah wa yote daima.” (59:22-23)

Tunaamini kuwa Allaah ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi:


لِّلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ‌ۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُ‌ۚ يَہَبُ لِمَن يَشَآءُ إِنَـٰثً۬ا وَيَهَبُ لِمَن يَشَآءُ ٱلذُّكُورَ  أَوۡ يُزَوِّجُهُمۡ ذُكۡرَانً۬ا وَإِنَـٰثً۬ا‌ۖ وَيَجۡعَلُ مَن يَشَآءُ عَقِيمًا‌ۚ إِنَّهُ ۥ عَلِيمٌ۬ قَدِيرٌ۬


“Ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anaumba Atakavyo. Humtunukia Amtakaye wana wa kike na Humtunukia Amtakaye wana wa kiume au Huwachanganya [wana wa] kiume na wa kike na Humjaalia Amtakaye kuwa ni tasa, hakika Yeye ni Mjuzi wa yote daima, Muweza wa yote daima.” (42:49-50)


لَيۡسَ كَمِثۡلِهِۦ شَىۡءٌ۬‌ۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ , لَهُ ۥ مَقَالِيدُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ‌ۖ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُ‌ۚ إِنَّهُ ۥ بِكُلِّ شَىۡءٍ عَلِيمٌ۬


“Hakuna chochote kinachofanana Naye - Naye ni Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima. Ni Zake Pekee funguo za mbingu na ardhi, Anamkunjulia riziki Amtakaye na Anamdhikisha [Amtakaye]. Hakika Yeye kwa kila kitu ni Mjuzi.” (42:11-12)

وَمَا مِن دَآبَّةٍ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ رِزۡقُهَا وَيَعۡلَمُ مُسۡتَقَرَّهَا وَمُسۡتَوۡدَعَهَا‌ۚ كُلٌّ۬ فِى ڪِتَـٰبٍ۬ مُّبِينٍ۬


"Na hakuna kiumbe chochote katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah; na Anajua makazi yake [tumboni mwa mama au duniani] na mahali pake pa kuhifadhiwa [baada ya kufa]. Yote yamo katika Kitabu kinachobainisha." (11:06)


وَعِندَهُ ۥ مَفَاتِحُ ٱلۡغَيۡبِ لَا يَعۡلَمُهَآ إِلَّا هُوَ‌ۚ وَيَعۡلَمُ مَا فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ‌ۚ وَمَا تَسۡقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعۡلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ۬ فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلۡأَرۡضِ وَلَا رَطۡبٍ۬ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ۬ مُّبِينٍ۬


“Na Kwake Pekee zipo funguo za mambo yaliyofichikana; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua. Na wala [haianguki] punje katika viza vya ardhi, na wala [hakianguki] kilichorutubika na wala [hakianguki] kikavu isipokuwa [kimeandikwa] katika Kitabu kinachobainisha.” (06:59)


إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُ ۥ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ ٱلۡغَيۡثَ وَيَعۡلَمُ مَا فِى ٱلۡأَرۡحَامِ‌ۖ وَمَا تَدۡرِى نَفۡسٌ۬ مَّاذَا تَڪۡسِبُ غَدً۬ا‌ۖ وَمَا تَدۡرِى نَفۡسُۢ بِأَىِّ أَرۡضٍ۬ تَمُوتُ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرُۢ


"Ana elimu ya Qiyaamah, na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika matumbo, na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote daima, Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana." (31:34)

Tunaamini kuwa Allaah anazungumza kwa yale ayatakayo, pale anapotaka na namna anavyotaka:


وَكَلَّمَ ٱللَّهُ مُوسَىٰ تَڪۡلِيمً۬ا


"Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno." (04:164)

وَلَمَّا جَآءَ مُوسَىٰ لِمِيقَـٰتِنَا وَكَلَّمَهُ ۥ رَبُّهُ


"Na alipokuja Muwsaa katika miadi yetu, na Mola wake Akamsemesha." (07:143)

وَنَـٰدَيۡنَـٰهُ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ ٱلۡأَيۡمَنِ وَقَرَّبۡنَـٰهُ نَجِيًّ۬ا 

"Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri." (19:52)


لَّوۡ كَانَ ٱلۡبَحۡرُ مِدَادً۬ا لِّكَلِمَـٰتِ رَبِّى لَنَفِدَ ٱلۡبَحۡرُ قَبۡلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَـٰتُ رَبِّى وَلَوۡ جِئۡنَا بِمِثۡلِهِۦ مَدَدً۬ا

“Kama bahari ingelikuwa ni wino wa [kuandika] maneno ya Mola wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu, japokuwa Tungelileta [bahari ya] mfano wake kuwa wino." (18:109)


وَلَوۡ أَنَّمَا فِى ٱلۡأَرۡضِ مِن شَجَرَةٍ أَقۡلَـٰمٌ۬ وَٱلۡبَحۡرُ يَمُدُّهُ ۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦ سَبۡعَةُ أَبۡحُرٍ۬ مَّا نَفِدَتۡ كَلِمَـٰتُ ٱللَّهِ‌ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ۬

"Na lau kama vile vyote vilivyomo ardhini kati ya miti [ingalikuwa] kalamu, na bahari [ikafanywa wino], ikaongezewa juu yake bahari saba [nyinginezo]; yasingelimalizika Maneno ya Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima, Mwenye hikmah wa yote daima." (31:27)

Tunaamini kuwa Maneno Yake ni matimilifu ya kweli katika kueleza, adilifu katika hukumu na ni mazuri. Amesema (Ta´ala):

وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدۡقً۬ا وَعَدۡلاً۬‌ۚ

"Na limetimia neno la Mola wako kwa kweli na uadilifu." (06:115)

وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ حَدِيثً۬ا

"Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?" (04:87)

قُلۡ نَزَّلَهُ ۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدً۬ى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ , وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّهُمۡ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ ۥ بَشَرٌ۬‌ۗ لِّسَانُ ٱلَّذِى يُلۡحِدُونَ إِلَيۡهِ أَعۡجَمِىٌّ۬ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِىٌّ۬ مُّبِينٌ

"Sema: Ameiteremsha roho Mtakatifu [Jibriyl] kutoka kwa Mola wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini na ni mwongozo na bishara kwa Waislamu. Na kwa yakini Tunajua kwamba wao [makafiri] wanasema: “Hakika [kuna] mtu [ndiye] anamfundisha [huyu Muhammad].” Lugha ya huyo wanayemnasibishia ni ya kigeni, na hii ni lugha ya kiarabu bayana." (16:102-103)

وَإِنَّهُ ۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ , نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلۡأَمِينُ  عَلَىٰ قَلۡبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُنذِرِينَ , بِلِسَانٍ عَرَبِىٍّ۬ مُّبِينٍ۬

"Na hakika hiyo ni Uteremsho wa Mola wa walimwengu. Ameiteremsha haya roho Mwaminifu juu ya moyo wako [ee Muhammad] ili uwe miongoni mwa waonyaji. Kwa lugha ya kiarabu bayana." (26:192-195)

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) Yuko juu ya viumbe Vyake kwa Dhati Yake na Sifa Zake. Amesema (Ta´ala):

وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ

"Naye ndiye Aliye juu, na ndiye Mkuu." (02:255)

وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦ‌ۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

"Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja Wake; Naye ni Mwenye hikmah wa yote daima, Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana." (06:18)

خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ۬ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ‌ۖ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَ‌ۖ

"Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akalingana juu ya ´Arshi. Huyaendesha mambo." (10:03)

Kulingana Kwake (Ta´ala) juu ya ´Arshi ni kuwa Kwake juu yake kwa Dhati Yake. Ni Ujuu maalum wenye kulingana na Utukufu na Ukubwa Wake na hakuna anayejua namna yake isipokuwa Yeye peke yake.

Tunaamini kuwa Yeye (Ta´ala) Yuko pamoja na viumbe Vyake na wakati huo huo Yuko juu ya ´Arshi Yake. Anazijua zali zao. Anayasikia maneno yao na anaona matendo yao. Anayaendesha mambo yao na anamruzuku fakiri. Anayarekebisha yenye kuvunjika na anampa ufalme Amtakaye na anamwondolea ufalme Amtakaye. Anamtukuza amtakaye na kumwangusha amtakaye. Kheri iko Mikononi Mwake na Yeye juu ya kila jambo ni Muweza.

Yule ambaye ana hadhi kama hii, anakuwa pamoja na waja Wake kihakika, hata
kama atakuwa pia juu ya viumbe Vyake kihakika.


لَيۡسَ كَمِثۡلِهِۦ شَىۡءٌ۬‌ۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye - Naye ni Mwenye kusikia yote daima,
Mwenye kuona yote daima.” (42:11)

Hatusemi kama wanavyosema Jahmiyyah na wakitaji (Huluuliyyah) wengine ya kwamba Allaah Yuko katika ardhi na viumbe Vyake. Tunaona kuwa mwenye kusema hivo ni kafiri au mpotevu, kwa sababu amemsifu Allaah kwa mapungufu yasiyolingana na Yeye.

Tunaamini yale Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyomweleza kwayo ya kwamba Hushuka kila usiku kwenye mbingu ya dunia kunapobaki thuluthi ya usiku ya mwisho na anasema:

"Ni nani mwenye kuniomba du´aa Nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba Nimpe? Ni nani mwenye kuniomba msamaha Nimsamehe?"

Tunaamini kuwa Yeye (Ta´ala) atakuja siku ya Qiyaamah kuhukumu kati ya waja. Amesema (Ta´ala):

كَلَّآ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكًّ۬ا دَكًّ۬ا , وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفًّ۬ا صَفًّ۬ا , وَجِاْىٓءَ يَوۡمَٮِٕذِۭ بِجَهَنَّمَ‌ۚ يَوۡمَٮِٕذٍ۬ يَتَذَڪَّرُ ٱلۡإِنسَـٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكۡرَىٰ

“Sivyo hivyo! [Kumbukeni pale] ardhi itakapovunjwavunjwa. Na Atakapokuja Mola wako na Malaika safusafu. Na utaletwa siku hiyo [Moto wa] Jahannam; siku hiyo mwanaadamu atakumbuka, lakini wapi atapata ukumbusho?” (89:21-23)

Tunaamini kuwa Anafanya alitakalo:

فَعَّالٌ۬ لِّمَا يُرِيدُ
”Afanyaye Alitakalo.” (85:16)

Tunaamini kuwa Yeye (Ta´ala) ana Utashi aina mbili:

Wa kilimwengu (Kawniyyah): Kwa Utashi huo kunapitika yale anayoyataka.

Pamoja na hivyo hailazimishi kwamba anayapenda. Katika hayo ni pamoja na Kauli Yake:

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقۡتَتَلُواْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يَفۡعَلُ مَا يُرِيدُ

“Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo."
(02:253)

إِن كَانَ ٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يُغۡوِيَكُمۡ‌ۚ هُوَ رَبُّكُمۡ

"Ikiwa Allaah Anataka kukuacheni kupotea. Yeye ndio Mola wenu." (11:34)

Ya Kishari´ah (Shar´iyyah): Utashi huo haulazimishi yapitike yale anayoyataka. Pamoja na hivyo yanalazimisha kwamba yale yenye kupitika anayapenda.

Amesema (Ta´ala):

وَٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡڪُمۡ

"Na Allaah Anataka kupokea tawbah kwenu." (04:27)

Tunaamini kuwa Matakwa Yake ya kilimwengu na ya Kishari´ah ni yenye kutokamana na Hekima Yake. Kila Anachokipanga kilimwengu au Kishari´ah waja wakaabudu kwacho, kinatokamana na Hekima, sawa tuwe tunajua Hekima hiyo au hatuijui:

أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَحۡكَمِ ٱلۡحَـٰكِمِينَ

”Je, kwani Allaah si Mbora wa wanaohukumu?” (95:08)

وَمَنۡ أَحۡسَنُ مِنَ ٱللَّهِ حُكۡمً۬ا لِّقَوۡمٍ۬ يُوقِنُونَ

”Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu; [Yanafahamika haya] kwa watu wenye yakini.” (05:50)

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) anawapenda mawalii Wake na wao wanampenda:

قُلۡ إِن كُنتُمۡ تُحِبُّونَ ٱللَّهَ فَٱتَّبِعُونِى يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡ‌ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬

"Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakusameheni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu." (03:31)

فَسَوۡفَ يَأۡتِى ٱللَّهُ بِقَوۡمٍ۬ يُحِبُّہُمۡ وَيُحِبُّونَهُ

"Allaah Ataleta watu Atakaowapenda nao watampenda." (05:54)


وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلصَّـٰبِرِينَ

"Na Allaah Anapenda wanaosubiri." (03:146)

وَأَقۡسِطُوٓاْ‌ۖ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

“Na fanyeni haki. Hakika Allaah Anapenda wafanyao haki.” (49:09)


وَأَحۡسِنُوٓاْ‌ۛ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ 

"Na fanyeni wema Hakika Allaah Anapenda wafanyao wema." (02:195)

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) anaridhia yale matendo na maneno Aliyoyaweka katika Shari´ah na kuchukia yale Aliyoyakataza:

إِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ عَنكُمۡ‌ۖ وَلَا يَرۡضَىٰ لِعِبَادِهِ ٱلۡكُفۡرَ‌ۖ وَإِن تَشۡكُرُواْ يَرۡضَهُ لَكُمۡ‌ۗ

“Mkikufuru, basi [eleweni kuwa] hakika Allaah ni Mkwasi kwenu na wala Haridhii kufuru kwa waja Wake. Na mkishukuru Huridhika nanyi.” (39:07)

وَلَـٰكِن ڪَرِهَ ٱللَّهُ ٱنۢبِعَاثَهُمۡ فَثَبَّطَهُمۡ وَقِيلَ ٱقۡعُدُواْ مَعَ ٱلۡقَـٰعِدِينَ

"Lakini Allaah Amechukia kutoka kwao, basi Akawazuia na ikasemwa: “Kaeni [mbakie majumbani] pamoja na wanaokaa.” (09:46)

Tunaamini kuwa Allaah Yuko radhi na wale wenye kuamini na kutenda matendo mema:

رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنۡہُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُ‌ۚ ذَٲلِكَ لِمَنۡ خَشِىَ رَبَّهُ

“Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye; hayo ni kwa yule anayemkhofu Mola wake.” (98:08)

Tunaamini kuwa Allaah anawaghadhibikia makafiri na wengine wenye
kustahiki kufanyiwa hivo:

ٱلظَّآنِّينَ بِٱللَّهِ ظَنَّ ٱلسَّوۡءِ‌ۚ عَلَيۡہِمۡ دَآٮِٕرَةُ ٱلسَّوۡءِ‌ۖ وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡہِمۡ

“Wanaomdhania Allaah dhana ovu utawafikia mgeuko uovu; na Allaah Awaghadhibikie.” (48:06)


مَن ڪَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ إِيمَـٰنِهِۦۤ إِلَّا مَنۡ أُڪۡرِهَ وَقَلۡبُهُ ۥ مُطۡمَٮِٕنُّۢ بِٱلۡإِيمَـٰنِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلۡكُفۡرِ صَدۡرً۬ا فَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٌ۬ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٌ۬

"Atakayemkufuru Allaah baada ya iymaan yake [atapata adhabu] isipokuwa yule aliyetenzwa nguvu na huku moyo wake umetua juu ya iymaan. Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu." (16:106)

Tunaamini kuwa Allaah Yuko na Uso. Ni Wenye kusifika kwa Utukufu na Ukarimu:


“Na utabakia Uso wa Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu.” (37:39)

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) ana Mikono miwili mikunjufu na mikubwa:

بَلۡ يَدَاهُ مَبۡسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيۡفَ يَشَآءُ‌ۚ

"Bali Mikono Yake iwazi Hutoa Atakavyo." (05:64)


وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦ وَٱلۡأَرۡضُ جَمِيعً۬ا قَبۡضَتُهُ ۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَـٰمَةِ وَٱلسَّمَـٰوَٲتُ مَطۡوِيَّـٰتُۢ بِيَمِينِهِۦ‌ۚ سُبۡحَـٰنَهُ ۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

”Na hawakumthamini Allaah kama inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata [Mkononi Mwake] Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kutokana na yale yote wanayomshirikisha.” (39:67)

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) ana Macho mawili ya kihakika. Amesema (Ta´ala):

“Na unda jahazi mbele ya macho Yetu na ufunuzi wa Wahy Wetu." (05:50)

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamekubaliana juu ya kwamba Ana Macho mawili. Jambo lenye kutilia nguvu hilo ni kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu ad-Dajjaal:

"Ana jicho moja na Mola Wenu hana Jicho moja."

Tunaamini kuwa:

لَّا تُدۡرِڪُهُ ٱلۡأَبۡصَـٰرُ وَهُوَ يُدۡرِكُ ٱلۡأَبۡصَـٰرَ‌ۖ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلۡخَبِيرُ

"Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho [yote]; Naye ni Mwenye kuyaendesha mambo kwa utuvu, Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana." (06:103)

Tunaamini kuwa waumini watamuona Mola Wao siku ya Qiyaamah:

وُجُوهٌ۬ يَوۡمَٮِٕذٍ۬ نَّاضِرَةٌ , إِلَىٰ رَبِّہَا نَاظِرَةٌ۬

“[Kuna] nyuso siku hiyo zitanawiri. Zikimtazama Mola wake.” (75:22-23)

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) hana wa kufanana Naye, kutokana na ukamilifu wa Sifa Zake:

لَيۡسَ كَمِثۡلِهِۦ شَىۡءٌ۬‌ۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye - Naye ni Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima.” (42:11)

لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬‌ۚ

“Haumchukuwi usingizi wala kulala.” (02:255)

Tunaamini kuwa hamdhulumu yoyote, kutokanana ukamilifu wa uadilifu Wake:

Vilevile tunaamini kuwa si Mwenye kughafilika na matendo ya yeyote katika waja Wake, kutokana na ukamilifu wa uchungaji na ujuzi Wake.

Tunaamini kuwa hakuna chenye Kumshinda mbinguni na ardhini, kutokana na ukamilifu wa ujuzi na uwezo Wake:

إِنَّمَآ أَمۡرُهُ ۥۤ إِذَآ أَرَادَ شَيۡـٴً۬ـا أَن يَقُولَ لَهُ ۥ كُن فَيَكُونُ

"Hakika Amri Yake Akitaka kitu chochote, hukiambia: “Kuwa!” nacho huwa." (36:82)

Hafikiwi na kitu kuchoka wala ushindwi, kutokana na ukamilifu wa nguvu Zake:

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ۬ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ۬

“Na kwa yakini Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, na wala Haukutugusa uchovu wowote.” (50:38)

Bi maana hakuhisi kuchoka wala kutaabika.

Tunaamini kuthibiti Majina na Sifa zote ambazo Allaah amejithibitishia Mwenyewe, au Majina na Sifa alizomthibitishia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo tunajitenga mbali na mambo mawili ya khatari:

1. Kulinganisha kwa kuamini au kwa maneno Sifa za Allaah na sifa za viumbe.

2. Kuziwekea namna kwa kuamini au kwa maneno ya kwamba Sifa za Allaah (Ta´ala) ziko namna fulani.

Tunaamini Allaah kutokuwa na kila kitu ambacho amejikanushia kuwa nacho, au kitu ambacho Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemkanushia kuwa nacho. ´Aqiydah hiyo ndani yake mna kuthibitishia kilicho kinyume chake. Vilevile tunanyamazia yale aliyoyanyamazia Allaah na Mtume
Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunaona kuwa kushikamana na mfumo huu ni jambo la lazima. Yale ambayo

Allaah amejithibitishia au kujikanushia Mwenyewe, ni maelezo ambayo Allaah amejithibitishia Mwenyewe. Yeye (Subhaanah) ni Mjuzi zaidi wa Nafsi Yake na  ni Mkweli zaidi wa usemi na ni Mwenye usemi mzuri kabisa, wakati waja Wake hawawezi kumzunguka kwa ujuzi. Vilevile yale aliyomthibitishia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au akamkanushia, ni maelezo aliyomweleza kwayo. Hakika yeye ni kiumbe mjuzi zaidi kuhusu Mola Wake, mtoaji nasaha,
mwaminifu na mfaswaha zaidi.

Katika Maneno ya Allaah (Ta´ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mna ujuzi kamilifu, ukweli na ubainifu zaidi. Hivyo hakuna udhuru kwa kuyarudisha au kuyatilia shaka kuyakubali.