´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn



Himdi zote anastahiki Allaah Pekee. Swalah na salaam ziwe juu ya yule ambaye hakuna Nabii mwingine baada yake, kizazi chake na Maswahabah zake.

Amma ba´d:

Nimepitia ´Aqiydah ilio nzuri na yenye kutosheleza ambayo imeandika ndugu yetu ´Allaamah muheshimiwa Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn.

Nimeisikia yote na kuona kuwa imebainisha ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika mlango wa Tawhiyd ya Allaah na Majina na Sifa Zake, katika mlango wa imani ya kuwaamini Malaika, Vitabu, Mitume, siku ya Mwisho na Qadar; kheri na shari yake.

Amefanya vizuri kuikusanya na amenufaisha. Humo ametaja yale anayoyahitajia mwanafunzi na kila muislamu katika imani yake ya kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Wake, Mitume Wake, siku ya Mwisho na Qadar; kheri na shari.

Ameongezea juu ya hayo faida zinazohusiana na ´Aqiydah ambazo huenda zisipatikane katika vitabu vingi vilivyoandika kuhusiana na ´Aqiydah.

Allaah amjaze kheri na amzidishie elimu na uongofu. Allaah anufaishe kupitia kitabu chake hichi na vitabu vyake vingine vyote. Allaah atujaalie sisi, yeye na ndugu zetu wengine wote tuwe katika waongofu wenye kuongoza wanaolingania katika dini ya Allaah kwa ujuzi. Hakika Yeye ni Msikivu,
yukaribu.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

Imeandikwa na kiumbe fakiri wa Allaah:

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz - Allaah amsamehe - ambaye ni Muftiy wa Saudi Arabia.